Usafi wa mazingira ulioboreshwa

Usafi wa mazingira bora ni neno ambalo linatumiwa kutofautisha aina au ngazi ya Usafi wa mazingira kwa lengo la ufuatiliaji. Neno hili liliundwa na Mpango wa ufuatiliaji wa pamoja (JMP) kwa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira wa UNICEF na WHO katika mwaka wa elfu mbili na mbili ili kusaidia kufuata maendeleo kuelekea lengo la saba la Malengo ya maendeleo ya milenia (MDG). Neno kinyume la “usafi wa mazingira ulioboreshwa” ni “usafi wa mazingira ambayo hajaboreshwa” katika ufafanuzi wa JMP.

Mpango wa ufuatiliaji wa pamoja (JMP) kwa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira huchapisha habari za hali ya usafi wa mazingira duniani kila mwaka. Kwa mfano, katika mwaka wa elfu mbili na kumi na tano iliripotiwa kwamba asilimia sitini na nane ya idadi ya watu duniani ilikuwa na upatikanaji wa usafi wa mazingira ulioboreshwa.[1]

Katika mwaka wa elfu mbili na kumi na saba, JMP iliunda neno jipya: “huduma ya msingi ya usafi”. Neno hili linatajwa kama matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo wa bora ambavyo hazikushirikiwa na kaya nyingine.

Kiwango cha chini cha huduma sasa inaitwa “huduma ya usafi ya ndogo” ambayo inahusu matumizi ya vifaa vya usafi ambavyo vimeboreshwa ambavyo ni vinatumia kati ya kaya mbili au zaidi.

Kiwango cha juu cha huduma inaitwa “usafi wa mazingira unaosimamiwa salama”. Hii ni aina ya huduma ya usafi wa msingi inahitajika kuwa salama katika situ au zinasafirishwa na kuchukuliwa mahali pengine.[2]

  1. Progress on sanitation and drinking-water : 2014 update. World Health Organization., UNICEF. Geneva. ISBN 9789240692817. OCLC 889699199.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
  2. Progress on drinking water, sanitation and hygiene : 2017 update and SDG baselines. World Health Organization,, UNICEF,. Geneva. ISBN 924151289X. OCLC 1010983346.{{cite book}}: CS1 maint: extra punctuation (link) CS1 maint: others (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne